MANAWASA kuwafikia w...
MANAWASA kuwafikia wananchi wengi zaidi
12 May, 2023
MANAWASA kuwafikia wananchi wengi zaidi

MANAWASA imepokea mabomba ya kusambaza huduma ya Maji kwa dhumuni la kuongeza mtandao wa maji kwa wakazi wa Wilaya ya Masasi na Nachingwea. Kupitia usambazaji wa  mabomba haya MANAWASA itaweza kuwafikia wakazi wengi zaidi walioko pembezoni mwa miji ya Masasi na Nachingwea na kero ya maji kwao itabaki historia. Tunawakaribisha wateja wetu kuchukua fomu za maombi ya huduma ya Majisafi.