Njia za Malipo

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA)  inatumia mfumo wa malipo wa kielektroniki wa Serikali (Government Elektronic Payment Gateway system – (GePGS) ambao umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa kuchakata Ankara za Maji (MAJIS) ambapo mteja upokea Ankara yake ya Maji kwa mwezi husika ikiambatana na kumbukumbu namba ya malipo (Control Number) yenye tarakimu 12. Kumbukumbu namba hiyo itatumika kila mwezi kwaajili ya  kulipia Ankara za maji kwani haibadiliki. Malipo ya Ankara ya Maji kutumia kumbukumbu namba ya malipo unaweza kulipa kwa njia ya mitandao ya simu za kiganjani au benki na mawakala wa benki pia. Wakati wa kufanya malipo, hatua zifuatazo zitatumika kutegemeana na mtandao.

Tigo-Pesa

Piga *150*01#
Bonyeza 4 Kulipia bili
Bonyeza 5 Malipo ya Serikali
Ingiza namba ya Malipo (Control Number, Mfano 995260182345)
Weka Kiasi
Ingiza Namba ya Siri
Bonyeza 1 Kuthibitisha

Halopesa

Piga *150*88#
Bonyeza 4 Kulipia bili
Bonyeza 5 Malipo ya Serikali
Ingiza namba ya Malipo (Control Number, Mfano 995260182349)
Weka Kiasi
Ingiza Namba ya Siri
Bonyeza 1 Kuthibitisha

M-pesa

Piga *150*00#
Chagua 4 –Lipa kwa M-Pesa
Chagua 5 – Malipo ya Serikali
Chagua 1 Namba ya Malipo
Ingiza 1 Namba ya Malipo
Ingiza namba ya Malipo (Control Number Mfano: 995260196789)
Weka Kiasi
Ingiza Namba ya Siri
Bonyeza 1 Kuthibitisha

TTCL PESA

Piga *150*71#
Chagua 5 – Lipia Bili
Chagua 3 – Malipo ya Serikali
Ingiza kumbukumbu namba (Control Number mfano: 995260193456)
Ingiza kiasi
Ingiza namba ya siri

BENKI

Njia nyingine ni kutumia benki za CRDB, NBC, NMB na Wakala zake za FAHARI HUDUMA, NBC wakala na NMB Wakala.