Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Mteja wa Maji anawajibika kuilinda na kuhakikisha Mita ya Maji haiharibiwi wala kuibwa.
Bomba la Mteja linapopasuka mbele ya Mita ya Maji  mteja anawajibika kulitengeneza na kuzuia maji kumwagika lakini Bomba likipasuka nyuma ya Mita ya Maji MANAWASA wanawajibu wa kulitengeneza.
Huduma ya maji itarejea ndani ya masaa ishirini na nne (24) ya kazi.
Mteja anatakiwa kupata huduma ya maji ndani ya siku saba (7) za kazi.
Kwa kufika ofisi za Manawasa Kupiga simu huduma kwa wateja 0788-446561 (Masasi) na 0786-727390 (Nachingwea) kuwasilisha lalamiko kupitia Sanduku la maoni lilipo kwenye ofisi za Manawasa Kwa njia ya barua.
Mteja anatakiwa kuwa na viambatanisho vifuatavyo; Picha moja Passport size (yenye rangi ya blue nyuma) Nakala ya kitambulisho kimoja wapo kati ya;  kitambulisho cha Taifa,Kitambulisho cha mpiga kura,Kitambulisho cha kazi  na leseni ya udereva.
Unaweza kulipa bili yako ya Maji kwa kutumia njia ya simu ya mkononi kupitia huduma ya Tigo Pesa, Airtel Money, M-pesa, Halopesa na T-pesa.
Piga *152*00# Chagua no.6 maji Chagua no.1 huduma za Pamoja Utachagua huduma unayoitaka Utafuata maelekezo, mfano ukichagua no.6 ulizia bili utatakiwa kuweka akaunti namba ili kuweza kupata bili yako.