Huduma ya Majisafi

 

Mamlaka inatoa huduma ya maji safi na salama kwa  wateja wa majumbani,Taasisi, Biashara,viwanda na wananchi katika Miji ya Masasi,  Nachingwea, na vijiji vya Masasi, Nachingwea na Ruangwa vilivyopo pembezoni mwa bomba kubwa linalotoka kwenye chanzo cha maji Mbwinji.  Pia Mamlaka inatoa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa mji wa Mangaka wilayani Nanyumbu kwa kuzingatia miongozo iliyopo; The water supply and sanitation(Quality of Services) Rules,2016 na Mkataba wa huduma kwa wateja.