Shughuli za Mazingira

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) ina wajibu wa kutunza mazingira ya vyanzo vya Maji  na inatekeleza jukumu hilo kwa  kupanda miti kila mwaka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji sambamba na kutoa  elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi  yakutojihusisha na shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya vyanzo vya maji kama kukata miti, kuchoma moto misitu, kuendesha shughuli za kilimo, kulisha mifugo na uchimbaji wa madini kwenye vyanzo vya maji . Mamlaka inashirikiana na wadau mbalimbali  wa mazingira katika kuimarisha ulinzi na usalama wa vyanzo vya maji kama vile  BONDE  LA RUVUMA NA PWANI YA KUSINI,Jumuiya ya Watumia maji Bonde la Ndanda (JUWABONDA), Tanzania Forest Service Agency (TFS) na vyombo vya usalama .