Chanzo cha Maji cha Mwena ni chanzo cha chemchemi ambacho uwezo wake ni lita 720,000 kwa siku na uzalishaji halisi wa kila siku ni lita 433,000 . Chanzo hiki kinahudumia baadhi ya vijiji vilivyo kando ya bomba kuu linalokwenda Mji wa Masasi ambavyo ni; Mbaju, Chisegu, Mandiwa, Chikukwe, Namakongwa, Chikundi na Mailisita. Wanainchi wa maeneo tajwa wanapata huduma ya majisafi na salama kutoka katika chanzo cha chemichemi za Mwena.