Wateja wanazohaki mbalimbali zilizoanishwa na pia wanawajibika kwa Mamlaka katika kutekeleza mambo mbalimbali kama yalivyoainshwa hapo chini.
- Kulipa ankara za maji kwa wakati.
- Kutoa ushirikiano kwa watumishi wanaowahudumia
- Kutoshawishi watumishi ili mteja ahudumiwe kwa upendeleo.
- Kuhudhuria mikutano au miadi kwa wakati uliopangwa.
- Kutoa taarifa sahihi zinazotakiwa kwa usahihi na kwa wakati unaotakiwa.
- Kuzingatia taratibu za kisheria kwa huduma zozote wanazostahili kupatiwa.
- Kufuatilia Ankara yake ya mwezi endapo hatapata .
- Kuwapokea wafanyakazi kwa heshima na unyenyekevu.
- Kutoa kwa wakati taarifa kamili na sahihi kwa kuzingatia aina ya huduma wanayohitaji kutoka Mamlaka.
- Kuheshimu amri na maelekezo ya MANAWASA na Mamlaka nyingine za usimamizi na udhibiti wa huduma za maji.
- Kutoa mrejesho juu ya huduma za Mamlaka pale ambapo matarajio yanakuwa hayajakidhiwa kwa muda mwafaka bila uoga wala kisasi.
- Kuhakikisha miundombinu ya maji kwenye eneo lako na hata maeneo mengine hayavuji.
- Kutoa taarifa kwa Mamlaka juu ya vitendo vyovyote vinavyohatarisha usafi na usalama wa maji.
- Kuzuia wizi, uharibifu na michepusho ya mita.
- Kutoa taarifa kwa Mamlaka juu ya mtumishi yeyote anayeendekeza vitendo vya rushwa.
- Mteja atawajibika na ulinzi wa dira ya maji iliyowekwa katika eneo lake, na endapo utatokea uharibifu wowote wa dira atagharamia mwenyewe.
- Mteja atawajibika kununua vifaa vya matengenezo ya bomba linalomuhudumia endapo utatokea uharibifu wowote ule.
- Kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mamlaka wanaowahudumia.
- Kutoa maoni kuhusu mipango na huduma zitolewazo na Mamlaka.
- Kutoharibu miundombinu ya majisafi na usafi wa mazingira.
- Kutoa taarifa kuhusu uharibifu wa miundombinu na vyanzo vya maji.
- Kutoa taarifa kuhusu uvujaji wa maji.