Malalamiko ya Wateja

Mteja atatoa lalamiko/malalamiko kwa kufuata taratibu zifuatazo;

1.Mteja atawasilisha malalamiko yake kwa kufika ofisi za MANAWASA,kupiga simu na kwa njia ya maandishi au kwa kujaza fomu zinazopatika katika ofisi ya huduma kwa wateja.

2.Baada ya mteja kuwasilisha malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku tano za kazi kama mkataba wa huduma kwa wateja unavyoeleza.

3.Pia Afisa huduma kwa wateja atawasiliana na mteja ili kufahamu kama tatizo limeshughulikiwa au bado.