Chemchemi za Mbwinji

Chanzo cha chemchemi ya Mbwinji kina chemichemi 3 ambazo ni Mbwinji, Rungwe na Minjale zenye uwezo wa kuzalisha lita 13,651,200 wakati wa kiangazi na uzalishaji halisi wa kila siku (wastani) wa lita 8,709,000 kwa siku. Chanzo hiki kinahudumia maeneo ya miji ya Masasi, Nachingwea, vijiji vilivyopo kandokando ya bomba kuu lakusambaza maji yanayotoka kwenye chanzo na vijiji 8 vilivyopo wilaya ya Ruangwa.