Chanzo cha Maji Mto Ruvuma
20 Feb, 2024

Mhandisi Asajile Ngoloke akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mh. Daktari Stephen Isaac Mwakajumilo kuhusu sehemu itakayowekwa mtego wa maji kwenye chanzo cha maji cha mto Ruvuma kilichopo kijiji cha Masuguru wilayani Nanyumbu.Kukamilika kwa chanzo hicho kitanufaisha wananchi wa Mji wa Mangaka na vijiji vilivyopo pembezoni mwa bomba kuu.