Ndugu Mteja.
Ninafurahi kuwakaribisha kwenye tovuti ya MANAWASA ambayo inaeleza kwa ufupi mambo mbalimbali ambayo taasisi yetu inafanya. MANAWASA inahudumia wateja kwa kutoa huduma ya Majisafi na Salama kwa wakazi wa miji ya Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na maeneo baadhi ya wilaya ya Ruangwa. MANAWASA ina watumishi wabobevu na wenye uwezo wa kusimamia kazi za kutoa huduma ya majisafi muda wote. Karibu sana MANAWASA TUKUHUDUMIE.